Mkutano wa Wikimania 2010

Kama jinsi ilivyo-ada. Kila mwaka kuna kuwa na mikutano ya Wanawikipedia wote wanakutana kujadili nini kifanyike baada ya mwaka kwisha. Mjadala mkubwa hasa ni uendelezi na upanuzi wa mradi wa Wikimedia Foundation na watoto zake, yaani, Wikipedia, Wikichuo, Wikamusi, Wikispishi, Wikihabari, Wikidondoo, na kadhalika. Wikimania humanishaa kwamba "Wiki na zana za Kiwiki, yaani, mfumo tunaotumia au Wikitext za kiwiki kwa ajili uchangizi wa makala na habari nyinginezo". Halafu "MANIA" kutoka Kiingereza: Kupenda sana kitu - kwa maana hiyo hawa wote wanaoshiriki katika mkutano huu ni wapenda Wiki ndiyo sababu wanaita Wikimania! Taarifa ni kwamba mwaka huu mutano unafanyika mjini GdaƄsk, Poland. Mikutano ya awali ilifanyika hapa: Buenos Aires, Argentina (2009) Alexandria, Egypt 2008) Taipei, Republic of China on Taiwan (2007) Cambridge, Massachusetts (2006) Frankfurt, Germany (2005) . Basi tangu ufanyika mkutano wa kwanza huko mjini Franfurt Ujerumani, kumekuwa na mfululizo wa mikutano hiyo kila mwaka. Tena kila mwenye kubahatika kuchaguliwa kwenda mkutanoni hupewa nafasi hiyo. Tangu mwaka wa jana, kumekuwa na kupewa kipaumbele kwa Waafrika kwenda huko kwa sababu waliowengi katika Afrika hawana uwezo wa kwenda nchi za mabali kama hizo. Hivyo, Wikimedia Foundation hutoa udhamini wa wachangiaji wake kwenda kushiriki katika mkutano. Basi kuwa mmoja wao!