Monday, May 10, 2010

Kutana na Ndesanjo Macha wa Wikipedia ya Kiswahili

Ndesanjo Macha ni mhariri wa zamani wa Wikipedia ya Kiswahili. Yeye, ni mmoja kati ya wale watu mwanzo kabisa waliokuwa wakichangia makala za Wikipedia ya Kiswahili. Alijiunga kwenye Wikipedia ya Kiswahili mnamo tar. 28 Septemba katika mwaka wa 2005.

Akiwa na jumla ya maharirio yote ni 1,022 mpaka mwezi wa Novemba katika mwaka wa 2009. Makala za kawaida ametunga kama 431 hivi - na alianza na makala yake ya kwanza ilikuwa Dodoma halafu Shilingi, mlima Kilimanjaro, Julius Nyerere, Mbege, Nchi za Maziwa Makuu, Fasihi, Intaneti, Blogu, Jua, na kadhalika! Kwa namna moja au nyingine, alikuwa mwanaharakati wa kweli (sina maana kaacha, la). Mpaka sasa bado anajishughulisha na masuala ya Shirika la Wikimedia, lakini katika nyanja za juu kabisa.

Huenda akawa Mswahili wa kwanza kufanya kazi na Wazungu wa Wikipedia ya Kiswahili. Hapo awali, alikuwa mpweke sana, lakini kiubishi, alisongesha!

Ndesanjo, ni mwandishi wa habari. Pia, ni mwanablogu wa kujitolea wa Global Voice (mkusanyiko wa wanablogu mbalimbali duniani). Lakini yeye yupo kwenye upande wa Kiswahili. Binafsi, ninakumbali vya kutosha!!! Na ninasema kaza buti!!!

Wenu,

Muddyb