Wednesday, April 21, 2010

Gerard Meijssen kutoka Uholanzi

Gerard Meijssen ni Mwanawikimedia pekee mwenye kuhangaikia masuala mengi ya uendelezi wa lugha za Kiafrika mtandaoni. Cheo chake mpaka sasa sikijui, lakini nilipata kumwuliza kwamba wewe ni nani kwenye Miradi ya Wikimedia - bureaucrat, steward au administrator, lakini akanijibu kwamba:

"No I am not. why would I, now I can choose what I do!"

Nikachoka kabisa. LAKINI pia nikagundua kwamba yeye ni kila kitu kwenye miradi ya Wikipedia kwa sababu anakuwepo kila mahali. Mpango wake hasa ni kuendeleza miradi hii ya Wikimedia na ndiyo maana habari zake yeye zinahusu Wikimedia tu, basi. Kwa upande mwingine pia, ni mmiliki wa mtandano wa OmegaWiki, MediaWiki Wave, The World Language Documentation Centre (WLDC), na ExtensionTesting. Pia, anapatikana mara kwa mara kule kwenye translatewiki.net na kazi yake hasa kutazama mabadiliko ya kusano zilizotafsiriwa kwa malugha mbalimbali. Kwa kweli, anastahili pongezi - kwa sababu huteletea habari hata kule kwenye Uswahilini juu ya maendeleo ya ufasiri wa kusano hizo kwa lugha Kiswahili.