Tuesday, November 10, 2009

Utangulizi

Habari,

Ninaitwa Mohamed au wengi huniita "Muddyb Blast". Ninatokea Dar es Salaam, Tanzania. Mimi ni mrasimu na msimamizi kwenye Wikipedia ya Kiswahili, kazi zangu nyingi nikiwa kwenye Wikipedia, ni kuandika makala za muziki na filamu tu, basi. Mengineyo, hubabaishia, lakini hasa muziki na filamu! Ukiwa una swali lolote kuhusiana na Wikipedia, basi niulize na itakuwa furaha yangu kukujibu swali lako kuhusu Wikipedia ile. Lengo langu la kufungua blogu hii ni kwa sababu ninataka kuipatia kujulikana Wikipedia ya nyumbani kwangu. Hasa kwa kuwa Wikipedia yenyewe bado ni changa - ilhali ni ya kwanza katika Afrika! Ukitazama Mawikipedia mengine kama ya Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, na nyinginezo nyingi. Utakuta sisi angalau tunajikusanya - wakati ile ya Kiingereza imefikisha makala 3,00,000 na kitu. Kwa sasa sina mengi, ila hapo baadaye, aah ni furaha tu... Wenu,

Muddyb